Home Simba SC KAZI NI KUBWA KWA SIMBA MBELE YA AS VITA MAMBO YAMEBADILIKA

KAZI NI KUBWA KWA SIMBA MBELE YA AS VITA MAMBO YAMEBADILIKA


 LEO Aprili kikosi cha Simba kitakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya AS Vita kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni hatua ya makundi.

Mchezo wa leo ni wa tano kwa Simba iliyo kundi A ambapo inahitaji pointi moja kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali na wapinzani wao AS Vita nao wanahitaji pointi tatu ili kufufua matumaini ya kutinga hatua ya robo fainali.

AS Vita ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 4 na Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 10 hivyo ikipata sare ya aina yoyote kwa Simba matumaini ya kusonga mbele yanafifia jumlajumla.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ina kazi kubwa ya kusaka ushindi kwa Mkapa kwa sababu ikishindwa leo itakuwa imepoteza ile nguvu ya mechi zake nne ambazo ilifanya vizuri.

Kupata pointi moja unaweza kusema ni jambo jepesi lakini ni gumu kwa sababu kila mchezo una aina tofauti ya kusaka ushindi.

Ukitazama namna ambavyo AS Vita wameanza kwa kusuasua msimu huu bado wana jambo lao kwa sababu kundi limekuwa huru na kila mmoja ana nafasi ya kufuzu hatua ya rbo fainali.

Kwenye mechi za ugenini inaonekana kwamba AS Vita wanakuwa imara kuliko nyumbani kwa sababu hizo pointi nne zote wamevuna wakiwa ugenini.

Walilazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Al Ahly wakiwa ugenini na walishinda mabao 3-1 dhidi ya Al Merrikh wakiwa ugenini.

Ikumbukwe kwamba Simba ilipocheza na Al Merrikh ugenini iliambulia pointi moja hivyo hakuna umuhimu wa kuubeza mchezo wa leo kwa Simba ni lazima wajue kwamba wana kazi kubwa na ngumu kufikia malengo.

AS Vita wakimaliza mchezo wa leo wana mchezo mwingine mkononi dhidi ya Al Merrikh iliyo na pointi moja nafasi ya nne na watakuwa nyumbani huku Simba kete yao ya mwisho watamalizana na Al Ahly iliyo nafasi ya pili na pointi 7 watakuwa ugenini.

Kwenye maisha ya soka tunasema kwamba kila kitu kinawezekana ila Simba wamalizane na AS Vita kwa Mkapa mapema na waingie ndani ya uwanja kwa heshima na adabu.

SOMA NA HII  BAO LA MORRISON LIRURIDWE..LIRUDIWE..HATUJALIONA VIZURI

Rekodi yao inaweza kutibuliwa leo na kuwafanya wasahau ule mwanzo wao mzuri na rekodi zao tamu, kila la kheri wawakilishi wa bendera ya Tanzania kimataifa.