Home Uncategorized MKUDE AELEZEA MAENDELEO YA AFYA YAKE..DAKTARI SIMBA AFUNGUKA PIA.!!

MKUDE AELEZEA MAENDELEO YA AFYA YAKE..DAKTARI SIMBA AFUNGUKA PIA.!!

KIUNGO mkabaji wa Simba, Jonas Mkude amewaambia mashabiki wa timu hiyo kwamba, ameanza kuwa fiti wala wasiwe na presha.

Mkude alieleza kuwa maendeleo yake ni makubwa kuliko na alivyokuwa hapo awali hata kutembea ilikuwa shida kutokana na maumivu ambayo alikuwa akiyasikia katika vidole vya mguu wa kulia na nyama za paja.

“Nitarudi tena kufanya vipimo vya mwisho ndio vitaamua hatma yangu kama naweza kuendelea kufanya mazoezi na wachezaji wenzangu au kutumika katika mechi au niongeze tena ratiba ya mazoezi haya ya peke yangu,” alisema.

“Nafahamu mashabiki wa Simba wanataka kufahamu maendeleo yangu kifupi naendelea vizuri na ambacho nafanya wakati huu ni taratibu tu za kimatibabu kutoka kwa wataalamu ili niweze kupona kabisa na nikirudi uwanjani niwe tayari kwa kushindana,” alisema Mkude.

Daktari wa Simba, Yassin Gembe alisema; “tayari ameanza ratiba ya kufanya mazoezi mepesi ambayo si muda mrefu ataingia katika mazoezi ya kawaida ambayo yatakuwa ya kurudisha ufiti wake kama ilivyokuwa hapo awali kabla ya kuumia.”

Mkude aliumia katika mechi ya kirafiki dhidi ya Simba na KMC baada ya kujigonga na beki wa kulia Kelvin Kajili.

SOMA NA HII  BREAKING: MUKOKO MCHEZAJI BORA MWEZI OKTOBA NDANI YA LIGI KUU BARA