Home Uncategorized DU! MUSONYE WA CECAFA NI PASUA KICHWA KWELI KUSUSU SIMBA NA YANGA

DU! MUSONYE WA CECAFA NI PASUA KICHWA KWELI KUSUSU SIMBA NA YANGA


NICHOLAUS Musonye, Katibu Mkuu wa CECAFA amesema kuwa Simba na Yanga hata kama wangeshiriki wasingepata kitu.

Michuano ya Kagame imemalizika jana ambapo Azam FC ambao walikuwa mabingwa watetezi walivuliwa ubingwa na timu ya KCCA ya Uganda kwa kufungwa bao 1-0.

“Bado wasingeweza kufanya kitu kwa kuwa mashindano yameandaliwa na Serikali ya Rwanda na kila kitu kimelipwa hivyo hakuna tatizo lolote kwa Simba na Yanga kutoshiriki,” amesema.

Simba ilialikwa kwenye michuano ya Kagame iliomba kujitoa kutokana na kubwana na ratiba za maandalizi ya msimu  ujao sawa na Yanga ambao nao pia waliomba kujitoa pia.

SOMA NA HII  TFF KUMCHUKULIA HATUA EYMAEL MPAKA FIFA