Home Uncategorized SABABU YA KCCA KUNYAKUA UBINGWA WA KAGAME MIKONONI MWA AZAM FC YATAJWA

SABABU YA KCCA KUNYAKUA UBINGWA WA KAGAME MIKONONI MWA AZAM FC YATAJWA

ALLAN Okello, mshambuliaji wa timu ya KCCA ya Uganda amesema kuwa kilichowapa ubingwa wa kombe la Kagame ni kucheza wakiwa timu.

KCCA jana walitwaa ubingwa wa Kagame mbele ya mabingwa watetezi Azam FC kwa ushindi wa bao 1-0.

Okello amesema: “Tumekuwa mabingwa wapya hili kwetu ni jambo la furaha, kikubwa kilichotupa ubingwa ni ushirikiano kwani tulicheza tukiwa timu mwanzo mwisho,” amesma.

KCCA wamewavua ubingwa Azam FC ambao ndio walikuwa na kombe msimu uliopita baada ya kushinda mbele ya Simba kwa kuifunga mabao 2-1 uwanja wa Taifa.

SOMA NA HII  LEWANDOWSKI AYEYUSHA MATUMAINI YA CHELSEA KUTINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA