Home Uncategorized SAFARI YA MABINGWA WA TPL SIMBA KIMATAIFA INAKWENDA NAMNA HII

SAFARI YA MABINGWA WA TPL SIMBA KIMATAIFA INAKWENDA NAMNA HII

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limetoa ratiba ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika kwa msimu ujao wa 2019/20.

Mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC wamepangwa kuanza na UD do Songo ya Msumbiji na wataanzia ugenini. 

Kwa mujibu wa ratiba, mechi za kwanza za raundi ya kwanza zitapigwa kati ya Agosti 9, 10 na 11 huku mechi za marudiano zikipigwa kati ya Agosti 23, 24 na 25.

Endapo vigogo hao wa Tanzania watapenya kwenye hatua hiyo, wataingia kwenye raundi ya pili ambapo Simba itakutana na mshindi kati ya Nyasa Big Bullets dhidi ya FC Platinum. 

SOMA NA HII  KAGERE AFIKIRIA KUWEKA REKODI NYINGINE NDANI YA LIGI KUU BARA