Home Uncategorized SABABU YA AZAM FC KUKOSA UBINGWA WA KAGAME HII HAPA

SABABU YA AZAM FC KUKOSA UBINGWA WA KAGAME HII HAPA


BRUCE Kangwa, beki wa timu ya Azam FC amesema kuwa kilichowaponza kushindwa kutetea kombe la Kagame ni kushindwa kutumia nafasi walizozipata kwa umakini.

Azam FC ilifungwa bao 1-0 na KCCA kwenye mchezo wa fainali iliyochezwa nchini Rwanda na kuvuliwa ubingwa waliokuwa wanautetea.

Bruce Kangwa amesema:” Tulicheza kwa juhudi ndio maana tumefika hatua ya fainali, kikubwa kilichotuponza ni kutokuwa makini hicho tu ndicho kimetukosesha ubingwa,”.

SOMA NA HII  MUNEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA