Home Habari za michezo ROBERTINHO ATAMBA UKUBWA WA SIMBA, AWAPA NENO WACHEZAJI

ROBERTINHO ATAMBA UKUBWA WA SIMBA, AWAPA NENO WACHEZAJI

Tetesi za Usajili Simba

Kocha Mkuu wa Simba SC Roberto Oliveira ‘Robertinho, amewapongeza wachezaji wake kwa kuonyesha kiwango kizuri katika mchezo dhidi ya Singida Fountain Gate, uliopigwa juzi Jumapili (Oktoba 08).

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa katika Uwanja wa Liti mkoani Singida, ulishuhudia Wekundu hao wa Msimbazi wakiibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Mabao ya Said Ntibazonkiza na Moses Phiri, kila mmoja akiingia kambani mara moja, yaliipa timu hiyo ushindi mnono na kuipaisha hadi katika nafasi ya kwanza, ikiwa na pointi 15.

Robertinho amesema wachezaji wake walijituma kwa kiasi kikubwa kuhakikisha timu inapata ushindi.

Kocha huyo amesema pamoja na kikosi chake kukutana na mpinzani mwenye wachezaji wenye uwezo mzuri, lakini wachezaji wake walionyesha kiwango cha hali ya juu kilichosababisha kupata ushindi.

“likuwa mechi ngumu, Singida FG ni timu imara na ilitupa upinzani mkubwa lakini Simba SC ni kubwa zaidi na tumeonyesha hilo kwa vitendo.”

“Nawapongeza wachezaji wangu kwa kazi nzuri waliyofanya, nawapongeza pia mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi kuja kutupa sapoti wamechangia pakubwa ushindi huu,” amesema Robertinho.

Kikosi cha Simba SC kimerejea jijini Dar es salaam jana Jumatatu (Oktoba 09), huku wachezaji wakipewa mapumziko kufuatia ratiba ya Kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), ambayo itaanza Oktoba 9 hadi 17, mwaka huu.

Klabu hiyo imesema baada ya ratiba ya kalenda ya FIFA kumalizika, kikosi kitarejea kambini kujiandaa kwa mchezo wa ufunguzi wa Super League dhidi ya Al Ahly, utakaopigwa Oktoba 20, mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam.

SOMA NA HII  HUYU HAPA KOCHA BORA WA MWEZI JANUARI, MZUNGU WA SIMBA NA MALALE HAMSINI WAPIGWA KIKUMBO