Home Habari za michezo ALY KAMWE AWATUPIA KIJEMBE HIKI SIMBA PACOME AHUSISHWA

ALY KAMWE AWATUPIA KIJEMBE HIKI SIMBA PACOME AHUSISHWA

Afisa Habari wa Yanga SC Ally Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe, amesema kuwa kwao uongozi wanajisikia furaha kusikia na kuona kila baada ya mchezo unapomalizika, wachezaji wao wanajadiliwa akiwemo Maxi Nzengeli na Stephene Aziz Ki kutokana na ubora wao tofauti na timu nyingine wanalalamikiwa waamuzi.

Kauli hiyo huenda ikawa kama kijembe kwa wapinzani wao, Simba ambao juzi mjadala mkubwa ulikuwa bao walilofunga Singida Fountain Gate kukatiliwa na mwamuzi wa kati, Tatu Malogo.

Pia Singida Fountain Gate walilalamikia bao la pili walilofungwa na kiungo mshambuliaji, Mzambia, Moses Phiri ambalo wanadai mfungaji alikuwa eneo la kuotea. Katika mchezo huo, Simba ilishinda 1-2.

Huo ni mchezo wa pili mfululizo timu pinzani kulalamika kufungwa mabao ya kuotea, awali ilikuwa dhidi ya Tanzania Prisons ambapo bao la pili la Simba lililofungwa na John Bocco linatajwa mfungaji alikuwa eneo la kuotea, waliposhinda 1-3.

Akizungumza na Spoti Xtra, Kamwe alisema wanajivunia usajili bora ambao uongozi wao chini Rais Injinia Hersi Said wanajadiliwa kila baada ya mechi kutokana na ubora wao.

Kamwe alisema wanataka kuona wachezaji hao wakionesha ubora huo katika kila mchezo watakaoucheza, ili kuthibitisha ubora huo katika ligi na michuano ya kimataifa.

“Katika kila mechi ya Yanga ikiisha mjadala huwa ni kwa akina Pacome, Aziz Ki na wengineo, lakini kwa wenzetu mechi zao zikisha mjadala unakuwa kwa waamuzi.

“Hiyo inathibitisha ubora wa wachezaji wetu ambao tumewasajili msimu huu, tunataka kuona wachezaji wetu wakionesha ubora wao katika kila mchezo.

“Bila kuangalia wapinzani wenzetu wanafanya nini, sisi tunataka pointi tatu katika kila mchezo sambamba na soka safi la kuvutia mashabiki wetu,” alisema Kamwe.

SOMA NA HII  HIKI HAPA NDIO KINACHOENDA KUTOKEA KWA YANGA NA GAMONDI WAKE