Home CAF NAMUNGO WATAJA KINACHOWAFELISHA KIMATAIFA

NAMUNGO WATAJA KINACHOWAFELISHA KIMATAIFA

 


HEMED Morocco, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa amekuwa akishindwa kupata matokeo chanya kwa kukosa wachezaji wenye uzoefu katika mashindano ya kimataifa.

Namungo FC inawakilisha Tanzania katika mashindano ya Kombe la Shirikisho ikiwa hatua ya makundi na ipo kundi D.

Ikiwa imecheza mechi tatu imepoteza mechi zote na haijaambulia pointi ambapo ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Pyramids na mabao 2-0 dhidi ya Raja Casablanca na mchezo wake wa tatu ilifungwa bao 1-0 dhidi ya Nkana.

Morocco amesema:”Nimeona kwamba wachezaji wanajitahidi kusaka ushindi ila wanashindwa kutokana na wengi kutokuwa na uzoefu katika mashindano haya makubwa.

“Bado tuna mechi na tuna nafasi ya kufanyia kazi makosa ambayo tunayafanya hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti,”.

SOMA NA HII  WAKATI YANGA WAKIUUMA ANA NAMUNGO....LUSAJO ATAENDELEA KULA MKATE MKAVU LEO...?