Home Uncategorized YANGA HAINA PRESHA NA SIMBA, MIPANGO YAO IPO HIVI

YANGA HAINA PRESHA NA SIMBA, MIPANGO YAO IPO HIVI


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mbelgiji, Luc Eymael ameibuka na kusema kuwa hana presha na Simba kuwafuata katika hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la FA kwa kuwa tayari ameshawaandalia dawa.

Mbelgiji huyo ametoa kauli hiyo baada ya Simba kuifunga Azam FC mabao 2-0 katika mchezo wa Kombe la FA uliopigwa Julai Mosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ambapo nusu fainali ya wababe hao inatarajiwa kupigwa Julai 12, mwaka huu.


Eymael amesema kuwa anaamini utakuwa mchezo mgumu kwa kuwa Simba wataingia uwanjani wakiwa na hesabu za kulipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 kwenye mchezo wao uliochezwa Machi 8 Uwanja wa Taifa.

“Nimeona namna ambavyo mambo yatakuwa kwani kila mtu anajua kwamba utakuwa mchezo mgumu lakini nasi pia tupo tayari kwa kuwa uwezo tunao na tunahitaji kupata ushindi.

“Kikubwa kwa sasa ni kuwaandaa wachezaji wetu kuwa sawa kuelekea kwenye mechi zetu za za ligi baada ya kumaliza nina amini kwamba tutakuwa na muda wa kujiandaa vizuri,” amesema.

Yanga, Julai 5 itamenyana na Biashara United kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Uwanja wa Karume, Mara.

SOMA NA HII  MIQUISSONE MDOGO MDOGO KAMA HATAKI