Home Simba SC SIMBA WATUA DAR KUIVUTIA KASI YANGA

SIMBA WATUA DAR KUIVUTIA KASI YANGA


BAADA ya kikosi cha Simba jana Juni 26 kukamilisha mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Azam FC,  leo kikosi kimerejea Dar.


Ubao wa Uwanja wa Majimaji ulisoma Azam FC 0- 1 Simba na kuwafanya mabingwa hao watetezi kutinga hatua ya fainali.

Mchezo huo ulishuhudiwa na mashabiki wengi ambao walikuwa ni wakazi wa Songea pamoja na maeneo mbalimbali ikiwa ni Mafinga, Iringa, Makambako na Njombe.

Alikuwa ni Luis Miquissone dk 89 aliyepachika bao la ushindi akitumia pasi ya Bernard Morrison. 

Kwa sasa wachezaji wamepewa mapumziko mafupi kabla ya kurejea kambini rasmi kuanza maandalizi ya mchezo dhidi ya Yanga, Julai 3, Uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  BAADA YA KUPOKEA KICHAPO LEO....NABI AVUNJA UKIMYA YANGA...AFUNGUKA WALIMUANGUSHA...