Home Yanga SC JK – MABADILIKO YANGA YANAWEZA KUWA MAZURI AU MABAYA

JK – MABADILIKO YANGA YANAWEZA KUWA MAZURI AU MABAYA


ALIYEKUWA Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amewataka uongozi wa Yanga kuwa makini katika upande wa kutafuta makocha na wachezaji wa timu hiyo.

Kikwete ameyasema hayo wakati aliokuwa amepewa nafasi ya kuzungumza kama mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa klabu ya Yanga.

“Muwe makini kutafuta kocha na wachezaji, mabadiliko ya mara kwa mara yanaweza yakawa mazuri lakini pia yakawa mabaya,” alisema Kikwete.

Kikwete amesema umakini unahitajika eneo hilo ili inabidi wawe makini na sio kubadili kocha katikati ya msimu au kuachana na wachezaji mapema.

Wanachama wa Yanga wakinyosha mikono kama kukubali mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji na mabadiliko ya katiba katika mkutano mkuu wa klabu hiyo.Picha na Michael Matemanga

Pia Kikwete aliwataka wanachama wawe na subira kwa wachezaji na makocha wanaoenda Yanga.

“Wanachama pia muwe na subira, timu haiwezi kujengwa kwa haraka, lazima wote wazoeane ili timu iwe bora,” alisema Kikwete.

Kikwete pia aliwaambia Uongozi wa Yanga kuhakikisha wanawahudumia wachezaji wa Yanga kwa kuwapa stahiki zao kwa wakati.

“Wachezaji wapewe mishahara, posho zao kwa wakati hiyo itaondoa masuala ya kusema wanahujumu timu, Ng’ombe analishwa ili atoe maziwa,” alisema Kikwete.

Kikwete ameongeza akisema;”Msipofanya hayo mtakuwa watu wa kamati ya ufundi na sio kamati ya benchi la ufundi, mambo hayo sio mazuri na ukiyaendekeza hautofikia mafanikio na uwekezaji mzuri kwenye timu ndio unaleta mafanikio.”

SOMA NA HII  AISEE!! NABI AZINYAKA SIRI ZA INONGA...AWAKABIDHI MAYELE NA MUSONDA...ISHU NZIMA HII HAPA A-Z