Home Yanga SC MANJI – NIMEACHA ROHO YANGU JANGWANI

MANJI – NIMEACHA ROHO YANGU JANGWANI

 


Mfadhili na mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Yusuf Manji amewambia wana Yanga kuwa amerudi nyumbani.

Manji aliombwa na wanachama apewe nafasi ya kuwasalimia baada ya hotuba ya mgeni rasmi, Jakaya Kikwete kwenye mkutano mkuu wa Yanga unaoendelea jijini Dar es Salaam.

Baada ya Dk Kikwete kumaliza hotuba yake, wanachama walipaza sauti wakiomba Manji awasalimie na mshareheshaji alirudhia.

Manji alitumia sekunde kadhaa kuwasalimia Wanayanga ambapo alianza kwa kuwasalimia na kuwaeleza muda mrefu hawajazungumza na wanachama kuitikia ndio huku wakishangilia na kisha kuwa watulivu kumsikiliza, ambapo aliwambia amerudi nyumbani.

“Kati ya viti nimeacha Jangwani (yalipo makao makuu ya Klabu ya Yanga) ni roho yangu, nashukuru nipo na tutaendelea kuwa wote mbele ya safari,” amesema Manji kwa kifupi.

SOMA NA HII  WACHINA WAIMWAGIA YANGA MABILIONI YA PESA....SASA KUTAMBA CAF KIBABE...STORI IKO HIVI..