Home Habari za michezo SIMBA YAJIBU KILIO CHA MASHABIKI….KAZI KUANZA RASMI KESHO…CHAMA MAPEMA TU….

SIMBA YAJIBU KILIO CHA MASHABIKI….KAZI KUANZA RASMI KESHO…CHAMA MAPEMA TU….

Kikosi cha Simba kinafanya mazoezi jijini Mwanza kujiandaa na mechi tatu mfululizo za Ligi Kuu Bara zitakazopigwa Kanda ya Ziwa, benchi la ufundi na baadhi ya nyota wa timu hiyo wakiwahakikisha mashabiki wanaenda kuvuna pointi tisa za ugenini.

Simba itaanza duru la pilikesho Jumapili  kwa kuvaana na Geita Gold kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza kabla ya kwenda Mjini Bukoba kuumana na Kagera Sugara wiki ijayo na kurudi tena Mwanza kucheza dhidi ya KMC.

Msimu uliopita Simba ilipasuka Kaitaba na kocha mkuu wa timu hiyo Juma Mgunda na nahodha msaidizi Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ wamesema wamesikia kelele za mashabiki wao wanaotaka safari hii wafanye kweli na kuahidi hawatawaangusha kwenye mechi hizo.

Simba imeondoka na wachezaji wake wote isipokuwa Peter Banda na Israel Mwenda walio majeruhi, huku kiungo fundi na mkali wa kuasisti, Clatous Chama aliyekuwa kwao Zambia ameuwahi msafara huo.

Chama aliomba ruksa kwenda Zambia mara baada ya mchezo wa raundi ya pili ya Kombe la ASFC dhidi ya Eagle SC waliyoipasua mabao 8-0 na alitarajiwa kutua mapema jana kuungana na wenzake kwenye mazoezi ya mwisho.

Katika mazoezi ya Simba wiki hii kulikuwa na ushindani mkali kwa wachezaji kutokana na kukubaliana kwenye kikao chao kuwa mechi tatu za Kanda ya Ziwa wanakwenda kupambana na kurudi na pointi zote tisa.

Hussein ‘Tshabalala’ alisema kwenye duru la pili mechi zinakuwa ngumu kutokana na kila timu kuhitaji kufikia malengo iliyojiwekea mwanzo wa msimu.

“Tunahitaji kutetea ubingwa wa ligi tuliyoupoteza msimu uliopita na kuhakikisha hilo linawezekana tunakwenda kupambana mechi tatu za ugenini na kupata pointi zote tisa zote.

“Wachezaji tumekubaliana hakuna mechi ya nyumbani wala ugenini zote tunakwenda kucheza ili kupata ushindi kama ambavyo mashabiki wetu wanavyotaka kuona.

“Kama ilitokea changamoto msimu huu kwenye baadhi ya michezo ya ugenini hili halipo tena, wachezaji tumedhamiria kupata matokeo bora kwenye michezo yote msimu huu katika mashindano ya ndani pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.”

Kocha wa timu hiyo, Juma Mgunda alisema msimu uliopita miongoni mwa sababu zilizochangia Simba kushindwa kufanya vizuri ni kushindwa kupata ushindi kwenye michezo ya ugenini ila msimu huu wanakwenda kulibadilisha hilo.

Mgunda alisema kuna kazi kubwa kwa wachezaji, benchi la ufundi na hata mashabiki wanatakiwa kuungana ili kupata ushindi kwenye michezo hiyo mitatu.

“Msimu uliopita Simba ilishindwa kufanya vizuri kwenye mechi tatu za ugenini mfululizo dhidi ya Mbeya City, Kagera Sugar na Mtibwa, na kushindwa kufikia malengo,” alisema Mgunda na kuongeza;

“Wachezaji wote wapo kwenye morali kubwa na kila mmoja anafahamu tunatakiwa kwenda ugenini kutafuta pointi tatu kwenye michezo hiyo ambayo itakuwa na ushindani mkali dhidi yetu.”

Simba inatarajiwa kucheza mchezo wa kwanza dhidi ya Geita keshokutwa Jumapili kisha kuumana na Kagera Desemba 21 na siku ya Boxing Day itavaana na KMC.

Kikosi cha Simba kinafanya mazoezi jijini Mwanza kujiandaa na mechi tatu mfululizo za Ligi Kuu Bara zitakazopigwa Kanda ya Ziwa, benchi la ufundi na baadhi ya nyota wa timu hiyo wakiwahakikisha mashabiki wanaenda kuvuna pointi tisa za ugenini.

Simba itaanza duru la pili Jumapili hii kwa kuvaana na Geita Gold kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza kabla ya kwenda Mjini Bukoba kuumana na Kagera Sugara wiki ijayo na kurudi tena Mwanza kucheza dhidi ya KMC.

Msimu uliopita Simba ilipasuka Kaitaba na kocha mkuu wa timu hiyo Juma Mgunda na nahodha msaidizi Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ wamesema wamesikia kelele za mashabiki wao wanaotaka safari hii wafanye kweli na kuahidi hawatawaangusha kwenye mechi hizo.

Simba imeondoka na wachezaji wake wote isipokuwa Peter Banda na Israel Mwenda walio majeruhi, huku kiungo fundi na mkali wa kuasisti, Clatous Chama aliyekuwa kwao Zambia ameuwahi msafara huo.

Chama aliomba ruksa kwenda Zambia mara baada ya mchezo wa raundi ya pili ya Kombe la ASFC dhidi ya Eagle SC waliyoipasua mabao 8-0 na alitarajiwa kutua mapema jana kuungana na wenzake kwenye mazoezi ya mwisho.

Katika mazoezi ya Simba wiki hii kulikuwa na ushindani mkali kwa wachezaji kutokana na kukubaliana kwenye kikao chao kuwa mechi tatu za Kanda ya Ziwa wanakwenda kupambana na kurudi na pointi zote tisa.

Hussein ‘Tshabalala’ alisema kwenye duru la pili mechi zinakuwa ngumu kutokana na kila timu kuhitaji kufikia malengo iliyojiwekea mwanzo wa msimu.

“Tunahitaji kutetea ubingwa wa ligi tuliyoupoteza msimu uliopita na kuhakikisha hilo linawezekana tunakwenda kupambana mechi tatu za ugenini na kupata pointi zote tisa zote.

“Wachezaji tumekubaliana hakuna mechi ya nyumbani wala ugenini zote tunakwenda kucheza ili kupata ushindi kama ambavyo mashabiki wetu wanavyotaka kuona.

“Kama ilitokea changamoto msimu huu kwenye baadhi ya michezo ya ugenini hili halipo tena, wachezaji tumedhamiria kupata matokeo bora kwenye michezo yote msimu huu katika mashindano ya ndani pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.”

Kocha wa timu hiyo, Juma Mgunda alisema msimu uliopita miongoni mwa sababu zilizochangia Simba kushindwa kufanya vizuri ni kushindwa kupata ushindi kwenye michezo ya ugenini ila msimu huu wanakwenda kulibadilisha hilo.

Mgunda alisema kuna kazi kubwa kwa wachezaji, benchi la ufundi na hata mashabiki wanatakiwa kuungana ili kupata ushindi kwenye michezo hiyo mitatu.

“Msimu uliopita Simba ilishindwa kufanya vizuri kwenye mechi tatu za ugenini mfululizo dhidi ya Mbeya City, Kagera Sugar na Mtibwa, na kushindwa kufikia malengo,” alisema Mgunda na kuongeza;

“Wachezaji wote wapo kwenye morali kubwa na kila mmoja anafahamu tunatakiwa kwenda ugenini kutafuta pointi tatu kwenye michezo hiyo ambayo itakuwa na ushindani mkali dhidi yetu.”

Simba inatarajiwa kucheza mchezo wa kwanza dhidi ya Geita keshokutwa Jumapili kisha kuumana na Kagera Desemba 21 na siku ya Boxing Day itavaana na KMC.

SOMA NA HII  CHELSEA YAZIDI KUKALIWA KOONI UINGEREZA...YAZUIWA KUSAJILI, KUUZA TIKETI ZA MECHI, WADHAMINI WAKIMBIA...