Home EURO 2020 ROONEY AMPIGA BENCHI GREALISH, AANZA NA RASHFORD DHIDI YA UJERUMANI

ROONEY AMPIGA BENCHI GREALISH, AANZA NA RASHFORD DHIDI YA UJERUMANI


MSHAMBULIAJI bora wa muda wote ndani ya kikosi cha England, Wyne Rooney amesema kuwa, kama  England inataka kupata ushindi dhidi ya Ujerumani kwenye mchezo wa Jumanne, basi kocha Gareth Southgate anatakiwa kumwanzisha benchi, kiungo mshambuliaji, Jack Grealish na kumuanzisha Marcus Rashford.

Grealish alionyesha kiwango kizuri katika mchezo wa mwisho wa makundi dhidi ya Jamhuri ya Czech, na kuwafanya watu wengi kuamini nyota huyo anapaswa kuanza kwenye mchezo wa Jumanne.

England na Ujerumani zinatarajiwa kukutana katika mchezo wa hatua ya 16, bora keshokutwa Jumanne, mchezo utakaopigwa katika dimba la Wembley.

Akizungumzia mawazo yake kuelekea mchezo huo Rooney alisema: “Licha ya kwamba nilimsifu Grealish kutokana na kiwango bora alichokionyesha dhidi ya Jamhuri ya Czech, lakini kwa mawazo yangu nadhani hapaswi kuanza kwenye mchezo wa Jumanne.

“Inabidi uwe na mbinu tofauti kuendana na wapinzani unaokutana nao, nadhani kwa namna ambavyo Ujerumani wanacheza mtu sahihi wa kuanza ni Marcus Rashford.”

SOMA NA HII  ITALIA YAIBAMIZA HISPANIA YATINGA FAINALI EURO 2020