Home EURO 2020 PERISIC ‘OUT’ CROATIA IKIWAVAA HISPANIA

PERISIC ‘OUT’ CROATIA IKIWAVAA HISPANIA

 


WINGA wa klabu ya soka ya Inter Milan na timu ya taifa ya Croatia, Ivan Perisic anatarajiwa kuukosa mchezo wa hatua ya 16 bora dhidi ya Hispania utakaopigwa kesho, kufuatia kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Jana Jumamosi jioni Shirikisho la soka la nchini Croatia (CFF), lilithibitisha taarifa za Perisic kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona. Huku nyota wengine na wafanyakazi wa kikosi hicho wakipimwa na kukutwa hawana maambukizi.

Nyota huyo Jumanne iliyopita alifunga bao katika ushindi wa mabao 3-1, walioupata Croatia dhidi ya Scotland uliowapa tiketi ya kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya Euro mwaka huu kutokea kundi D.

Taarifa ya CFF ilieleza: “Shirikisho la soka la Croatia Jumamosi jioni lilipokea majibu ya vipimo vya wachezaji wote ambayo yalieleza kuwa mchezaji, Ivan Perisic amekutwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

“Perisic aliondolewa mara moja kikosini na kutengwa na nyota wengine kwa ajili ya kuzuia kusambaa kwa ugonjwa, na sasa atakuwa na siku 10  za kujitenga.”

SOMA NA HII  ITALIA YATINGA NUSU FAINALI EURO 2020