Home Uncategorized SURE BOY AREJEA NDANI YA UWANJA

SURE BOY AREJEA NDANI YA UWANJA


SALUM Abubakar ‘Sure Boy’,kiungo mzawa anayekipiga ndani ya Azam FC ameanza mazoezi ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Aristica Cioaba.

Sure Boy alianza mazoezi jana, Uwanja wa Azam Complex na wachezaji wenzanke ambao wanajiaandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida United.

Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Chamazi majira ya saa 1:00 usiku.

Sure Boy alikuwa akisumbuliwa na majeraha ya kisigino, yaliyomuweka nje ya Uwanja takribani wiki mbili.

SOMA NA HII  MASTAA HAWA UANGA WAITAMANI SIMBA KUFA KUPONA DABI YA KARIAKOO