Home Uncategorized MABAO YA KASEKE YAACHA REKODI TAIFA

MABAO YA KASEKE YAACHA REKODI TAIFA


DEUS Kaseke, kiraka wa Yanga ameweka rekodi yake ndani ya dakika 180 kwa kufunga kwenye mechi mbili mfululizo mabao matatu kwenye lango la Kaskazini, Uwanja wa Taifa.
Kaseke alianza balaa lake Juni 27, Uwanja wa Taifa, wakati Yanga ikishinda mabao 3-2 mbele ya Ndanda mchezo wa Ligi Kuu Bara dakika ya 6 kwa pasi ya Ditram Nchimbi na 45 kwa pasi ya Juma Abdul yote kwa kichwa Uwanja wa Taifa.
Juni 30 alirejea tena kambani kwa kufunga bao dakika ya 76 kwa guu la kulia kwa penalti mbele ya Kagera Sugar kwenye ushindi wa mabao 2-1 kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali.
Bao hilo limeifanya Yanga kutinga hatua ya nusu fainali ambapo itakutana na Simba Uwanja wa Taifa, Julai 12.

Simba ilitinga hatua hiyo baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Azam FC.
Kaseke amekuwa kwenye ubora wake msimu huu ambapo kwenye mashindano yote jumla amefunga mabao matatu na pasi nne.
SOMA NA HII  BREAKING:AZAM FC YAMALIZANA NA MAKOCHA WATATU