Home news BAADA YA NKANE KUTUA YANGA…BIASHARA UTD WASHINDWA KUJIZUIA…WATOA KAULI NZITO…

BAADA YA NKANE KUTUA YANGA…BIASHARA UTD WASHINDWA KUJIZUIA…WATOA KAULI NZITO…


NAHODHA wa kikosi cha Biashara United, Abdulmajid Mangalo ameweka wazi kuwa anamtakia kila la kheri winga wa kikosi hicho, Denis Nkane kwenye dili lake la kujiunga na Yanga na anaamini uhamisho huo umestahili.

Nkane pamoja na Mkongomani, Chiko Ushindi ni miongoni mwa mastaa wawili ambao wapo kwenye mazungumzo ya mwisho ya kujiunga na Yanga katika dirisha hili dogo la usajili ambalo lilifunguliwa rasmi Desemba 16, mwaka huu.

Ikumbukwe hivi karibuni uongozi wa Biashara United uliweka wazi kuwa kwenye hatua nzuri ya mazungumzo ya uhamisho wa Nkane kujiunga na Yanga, huku aliyekuwa kocha wa Biashara, Patrick Odhiambo akikiri ni kweli Nkane anaondoka.

Akizungumza  Mangalo alisema: “Kama nahodha wa Biashara United najua wazi ubora alionao Nkane na mchango wake ndani ya kikosi chetu kwa kipindi chote ambacho amekuwa pamoja nasi, ni kweli kwa kiasi kikubwa tunatarajia ataondoka na kujiunga na Yanga.

“Sisi ni wachezaji na mpira ndiyo kazi yetu hivyo kama atafanikisha uhamisho wake sisi tunamtakia kila kheri katika majukumu yake mapya nami binafsi naamini kwa yale aliyoyafanya anastahili kujiunga na Yanga.”

SOMA NA HII  FT: SIMBA 3-0 GEITA GOLD.... OKRAH, PHIRI NA CHAMA WAFANYA YAO....'MZUNGUU' BADO SANA..AINGIA NA ZALI...