Home news NAMUNGO:TUMENYANYASWA KWELI KWA JAMBO AMBALO TUMEFANYIWA

NAMUNGO:TUMENYANYASWA KWELI KWA JAMBO AMBALO TUMEFANYIWA


UONGOZI wa Namungo umeweka wazi kuwa kwa kitendo walichofanyiwa na wenyeji wao Angola ni manyanyaso makubwa jambo ambalo limewafanya wasiwe na amani ndani ya mioyo yao.

Namungo ambao ni wawakilishi wa Tanzaia kwenye Kombe la Shirikisho walikuwa na kibarua cha kucheza mchezo wa hatua ya 32 bora dhidi ya 1 de Agosto ya Angola ambayo ni mali ya Wanajeshi.

Mchezo huo ambao ulipangwa kuchezwa Februari 14 ulifutwa na Shirikisho la Soka Afrika,(Caf) kutokana na wachezaji wa Namungo pamoja na viongozi kutakiwa kukaa karantini kwa muda kabla ya mchezo.

Pia wachezaji watatu na kiongozi mmoja walizuiwa kuwa kwenye msafara kwa kile ambacho kilielezwa kuwa wamekutwa na maambukizi ya Virusi vya Corona jambo ambalo limekuwa likipingwa na viongozi hao wakisema kuwa sio sawa.

Mpango wa Namungo kureja Bongo Februari 14 ulikwamba baada ya mamlaka ya Angola kuhitaji wachezaji hao watatu pamoja na kiongozi mmoja kubaki karantini jambo lililowasubirisha.

Jana Februari 15 walianza safari mchana na kuwasili Bongo usiku huku wakiwa wamewaacha wachezaji watatu pamoja na kiongozi mmoja wakiwa chini ya uangalizi wa Serikali ya Angola na wakimaliza utaratibu uliowekwa watareja Bongo kwa gharama za Serikali ya Angola.

Hassan Zidadu, Mwenyekiti wa Klabu ya Namungo FC amesema kuwa hawana furaha kwa kile walichofanyiwa kwa kuwa walinyanyaswa bila hatia.

“Tumenyanyaswa bila sababu kwa kuwa hakuna maelezo mazuri ambayo tulikuwa tunapewa, ndani ya mioyo yetu hatukuwa na amani kabisa na tunashukuru kwa dua za Watanzania,”. 


SOMA NA HII  WAKATI YANGA WAKIHANGAIKA NA SportPESA...CAF WAIPA KIBALI SIMBA KUTUMIA NEMBO YA M-BET..