Home Uncategorized ISHU YA ‘SUB’ 5 NDANI YA LIGI KUU BARA IMEKAA HIVI

ISHU YA ‘SUB’ 5 NDANI YA LIGI KUU BARA IMEKAA HIVI

 


MTENDAJI Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almas Kasongo amesema kuwa hakutakuwa na mabadiliko ya wachezaji watano kama ambavyo walitumia katika kumalizia ligi msimu uliopita.

 

Ligi nyingi duniani zilitumia mabadiliko ya wachezaji watano kupitia sheria ya dharula iliyotolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kwa ajili ya kusaidia ligi kumalizika vizuri baada ya kutoka kwenye mapumziko ya muda mrefu yaliyosababisha na janga la Ugonjwa wa COVID-19.

 

Kasongo ameliambia Championi Jumamosi kuwa, kuelekea msimu mpya wa ligi hakutakuwa na mabadiliko ya wachezaji watano kwa kuwa hapo awali walitumia idadi hiyo kutokana na dharula iliyojitokeza ya maambukizi ya Viurusi vya Corona, hivyo wao wataendelea na mabadiliko ya wachezaji watatu kama ilivyo kawaida.


“Sheria inayotambulika kwenye suala la mabadiliko ya wachezaji ni watatu, tulikuwa tukitumia idadi ya wachezaji watano kwenye mabadiliko msimu uliopita kwa sababu ya dharula ambayo iliikumba dunia nzima na kuathiri baadhi ya shuguli kama za michezo.

 

“Kikubwa waliona kuwa ligi zinarejea lakini wachezaji hawatakuwa fiti ndipo sheria ikawekwa ya kuongeza idadi kutoka watatu na kwenda watano hivyo dharula hiyo ishakwisha na kwetu hakuna mapendekezo yaliyokuja kuwa tuendelee na mabadiliko ya watu watano, hiyo ina maana kuwa tutaendelea kutumia wachezaji watatu kwenye mabadiliko,” alisema Kasongo.

SOMA NA HII  JOSE MOURINHO:USHINDI WA LIVERPOOL NI WA KUTENGENEZWA