Home Uncategorized KIPA YANGA AKODI KOCHA KENYA

KIPA YANGA AKODI KOCHA KENYA

KIPA wa Yanga, Farouk Shikhalo amesema baada ya kurejea mazoezini amechukua hatua ya kukodi kocha kwa muda wa kumpa mazoezi.

Kipa huyo wa Kenya amesema kuanzia wiki hii ameanza kupewa mazoezi na mmoja wa makocha wa nchini hapo  Yusuf Mohamed.

Shikhalo amesema kocha huyo atakuwa anamlipa kwa gharama zake kuhakikisha analinda ubora wake wakati huu akisubiri mipaka ya Kenya kufunguliwa ili aweze kurejea nchini baada ya kufungwa kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa COVID -19.

Amesema imekuwa kama bahati kumpata Mohamed ambaye anatoka eneo ambalo anaishi kutokana na wengi kutoruhusiwa kutembea umbali mrefu.

Amesema mbali na kocha huyo pia amepata kipa mwenzake anayecheza ligi ya kwao Kenya, Saeed Alele ambaye anafanya naye mazoezi.

Amesema ratiba yao utakuwa ni kufanya mazoezi hayo kwa saa moja na nusu mpaka mawili katika uwanja wa Serani jijini Mombasa.

Shikalo yupo kwao baada yaSerikali nchini kusimamisha shughuli zote zinazosababisha mikusanyiko ikiwemo ligi zote ambapo hadi sasa haifahamiki ligi hizo zitaendelea lini.

SOMA NA HII  MAPILATO WA AZAM FC KIMATAIFA HAWA HAPA