Home video VIDEO:MBOMBO AWEKA WAZI MIKAKATI NDANI YA AZAM FC, AWAITA MASHABIKI

VIDEO:MBOMBO AWEKA WAZI MIKAKATI NDANI YA AZAM FC, AWAITA MASHABIKI

IDRIS Mbombo mshambuliaji wa Azam FC ameweka wazi kuwa kwa kushirikiana na wachezaji wengine ndani ya kikosi hicho anaamini kwamba watafanya vizuri.


 Kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Septemba 11 ikiwa ni mara yake ya kwanza kucheza ndani ya uzi wa Azam FC katika mashindano ya kimataifa kwa kuwa ni ingizo jipya kwa msimu wa 2021/22, Mbele ya Horseed FC nyota huyo aliweza kupachika bao la pili dakika ya 73 na kuwanyanyua mashabiki wa Azam FC waliokuwa wakifuatilia mtanange huo kupitia Azam TV. 
Azam FC iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 3-1. Ameongeza kuwa uwepo wa Rodgers Cola na Prince Dube utawafanya waweze kufanya vizuri ni suala la mashabiki kuwa nao bega kwa bega.

 

SOMA NA HII  VIDEO:YANGA YAITANGAZIA VITA SIMBA, MORRISON AANDALIWA KUIUA AZAM FC