Home Habari za michezo YANGA KWELI NI BABA LAO….HUYU HAPA GOLIKIPA MKENYA ANAYETAMANI KUSAJILI JANGWANI MSIMU...

YANGA KWELI NI BABA LAO….HUYU HAPA GOLIKIPA MKENYA ANAYETAMANI KUSAJILI JANGWANI MSIMU UJAO…

 


Si ajabu mtu kuwa na ndoto, si jambo la kustaajabisha endapo mtu atakuwa anatamani Leo au kesho kupata kitu hiki au kile, huwa ajabu tu pale ambapo mtu anapokosa tamanio la kesho yake.

Katika kuonyesha thamani ya tamanio, kipa wa kikosi cha Posta Rangers inayoshiriki Ligi Kuu nchini Kenya FKFPL Kelvin Opiyo amesema ana ndoto za siku moja kucheza ndani ya uzi wa Timu ya Wananchi, Yanga.

Mlinda mlango huyo wa zamani wa Vihiga United na APS Bomet amesema pamoja na kuwa na wakati mzuri Posta Rangers lakini atabakia kuwa mwenye amani kwenye taaluma yake endapo atacheza Yanga au Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Akizungumza na moja ya chombo cha habari nchini Kenya katika kipindi hiki ambacho Ligi Kuu ya KPL Kenya imalizika, Opiyo ameelezea matamanio yake ya kuyafikia kwenye soka.

“Ndoto zangu ni siku moja kucheza Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns. Ningependa hata kucheza Yanga ya Tanzania”, alieleza mchezaji huyo ambaye mwishoni mwa Ligi alipoteza nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha Rangers.

Kuhusu ndoto za timu ya taifa ya Kenya, Opiyo ameeleza kuwa atakuwa hajatimiza ndoto zake kimpira endapo atashindwa kuitumikia timu ya taifa (Harambee Stars) maana ndiyo inayobeba wasifu wote kwa ujumla.

SOMA NA HII  WAKATI TETESI ZA MAYELE KUTAKIWA NA KAIZER CHIEFS ZIKIZIDI KUKUA...INJINIA HERSI AIBUKA NA HILI JIPYA....