Home Uncategorized MASHINE HIZI 6 SIMBA UHAKIKA, MABOSI WAMEMALIZANA NAO KILA KITU

MASHINE HIZI 6 SIMBA UHAKIKA, MABOSI WAMEMALIZANA NAO KILA KITU


HOMA ya Usajili ndani ya Ligi Kigi Kuu Bara inazidi kupanda huku vikumbo vikiongezeka kwa kila timu kuhitaji kufikia malengo yake.



Tayari Simba imewatangaza wachezaji wake sita ambao msimu ujao ni uhakika kuwa ndani ya kikosi hicho cha mabingwa wa Ligi Kuu Bara.

Hawa hapa mashabiki wana uhakika wa kuwaona wakiwa na jezi za Simba  kwa kuwa wamemalizana na Simba na wametangazwa rasmi:-

Meddie Kagere ameongeza mkataba wa miaka miwili ndani ya Simba, ana tuzo tatu za mchezaji bora ndani ya TPL, ni kinara wa utupiaji msimu uliopita akiwa amefunga mabao 23.

John Bocco, nahodha wa Simba, ameongezewa mkataba wa miaka miwili, ni mshambuliaji ambaye msimu uliopita alifunga mabao 16.

Erasto Nyoni, beki kiraka wa Simba, ameongezewa mkataba wa miaka miwii ni beki ambaye msimu wa 2018-19 ametwaa tuzo mbuiili za Simba ikiwa ni pamoja na bbeki bora na ile ya chaguo la wachezaji..

Aishi Manula, Mlinda mlango wa Simba, ameongezewa miaka mitatu,msimu wa 2018/2019, Aishi Manula amecheza michezo 30 ya Ligi Kuu na katika michezo 18 kati ya hiyo hajaruhusu bao lolote (cleansheet) 

Jonas Mkude, Kiungo wa Simba, ameongezewa mkataba wa miaka miwili ni kipenzi cha mashabiki wa Simba.

Beno Kakolanya, Mlinda mlango wa Simba amesajiliwa akiwa ni mchezaji huru baada ya kuvunjas mkataba na mabosi wake wa zamani Yanga.

SOMA NA HII  YANGA:TUNAWATAMBUA AKINA MKUDE, CHAMA, HATUNA PRESHA