Home Habari za michezo CHAMA KWISHA MANENO HANA JAMBO SIMBA DAKIKA ZAKE NI HIZI TU

CHAMA KWISHA MANENO HANA JAMBO SIMBA DAKIKA ZAKE NI HIZI TU

Habari za Simba SC

Mchezaji wa zamani wa Taifa Stars na vilabu vya Yanga na Simba, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ amesema kuwa, kiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama amechoka na hwezi tena kuwa na ubora ule ule kama ambao alikuja nao Simba mwaka 2018.

Jembe Ulaya amesema kuwa, Chama ameshafanya kila kitu anachotakiwa kufanya ndani ya Simba hivyo klabu hiyo wanapaswa wafanye maamuzi magumu ya kuondoa maadhi ya wachezaji na kusajili damu changa.

“Chama ameshafanya kila kitu kinachohitajika Simba, lakini kama wanataka kwenda kufanya makubwa kwenye Soka la Afrika wanapaswa waachane na baadhi ya wachezaji. Chama ni mchezaji mzuri lakini kwa sasa hawezi kukupa ubora uleule kwa dakika 90.

“Chama ni mchezaji ambaye unaweza kuwa naye kwa kucheza dakika 30 au 45. Benchikha sasa hivi ndiyo mwenye maamuzi ya mwisho,” amesema Jembe Ulaya.

SOMA NA HII  UONGOZI WA SIMBA WAFUNGUKA MAZITO KUHUSU PHIRI KUTOKUCHEZA