Home Habari za michezo UONGOZI WA SIMBA WAFUNGUKA MAZITO KUHUSU PHIRI KUTOKUCHEZA

UONGOZI WA SIMBA WAFUNGUKA MAZITO KUHUSU PHIRI KUTOKUCHEZA

Habari za Simba

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ amefunguka kuhusu sakata lililoibuliwa mitandaoni na mashabiki wa timu hiyo wakihoji kwa nini Kocha Robertinho hampi nafasi mshambuliaji wao, Moses Phiri licha ya kupona majeraha yake.

Try Again akizungumzia hilo amesema; “Usajili umefanyika kitaalamu kutokana na malengo na mipango ya timu, kusajili ni kitu kimoja ndani ya uwanja ni kitu cha pili, mwisho wa siku mwalimu ndio anaamua lakini pia utayari wa mchezaji mwenyewe mazoezini pia kuna injury na vitu vingine vingi,” amesema Salim Try Again.

Tangu ujio wa kocha Robertinho, Phiri hajapata nafasi ya kuanza kwenye kikosi chake hata kwa zile mechi za kawaida na zile za kirafiki licha ya kufunga mabao 10 katika nusu tu ya msimu alipojiunga na miamba hao wa soka jambo ambalo limewafanya mashabiki kucharuka hasa baada ya kunyimwa nafasi kwenye mechi dhidi ya Power Dynamos kwenye Simba Day Jumapili iliyopita.

SOMA NA HII  GAMONDI HUYU ANATAKA KUFUATA NYAYO ZA MANARA!?