Home Habari za michezo KUELEKEA MSIMU MPYA WA LIGI KUU…SIMBA NA YANGA ZAWEKWA KWENYE ‘KONA MAALUMU’…

KUELEKEA MSIMU MPYA WA LIGI KUU…SIMBA NA YANGA ZAWEKWA KWENYE ‘KONA MAALUMU’…

Yanga SC na Simba SC

Kocha Mkuu wa Tabora United, Goran Copnovic amesema kikosi chake kitatoa upinzani mkubwa kwa timu za Simba SC na Young Africans kwenye Ligi Kuu ya msimu ujao kutokana na usajili walioufanya.

Miongoni mwa usajili wa nguvu uliofanywa na Tabora United ni Mlinda Lango wa Mabingwa wa Soka nchini Nigeria Enyimba, John Noble ambaye pia alikuwa akiwaniwa na klabu ya Simba SC.

Kocha huyo aliyewahi kuifundisha klabu ya Simba SC miaka ya nyuma amesema anatambua atakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa klabu za Simba SC na Young Africans, lakini yupo tayari kupambana nazo na anaamini ataibuka mshindi mbele yao.

“Simba SC na Young Africans ndio wapinzani wangu wakubwa katika mafanikio ambayo tumekusudia kuyafikia lakini usajili ambao tumeufanya unanipa nguvu ya kupata kile tulicho kikusudia ambacho ni kumaliza ligi kwenye nafasi za juu ikiwemo ubingwa wa Ligi Kuu.” amesema Kocpnovic.

Kocha huyo raia vwa Serbia amesema mpaka sasa maandalizi yao kuelekea msimu ujao yanakwenda vizuri na mechi za kirafiki wanazoendelea kucheza zimempa mwanga wa kujua wachezaji gani wa kuwatumia kwenye kikosi chake cha kwanza.

Amesema pamoja na ugeni wao, lakini ameandaa mifumo maalumu ya uchezaji kuhakikisha wanahimili ushindani na kufikia malengo yao.

Hiyo itakuwa mara ya kwanza kwa Tabora United kushiriki Ligi Kuu, baada ya kupanda msimu uliopita ikitokea ligi ya Charnpionship pamoja na timu za Mashujaa FC na JKT Tanzania.

SOMA NA HII  KILICHOTOKEA JANA, SIMBA NA YANGA HAWAWEZI