Home Habari za michezo FEI TOTO ATOA NENO HILI BAADA YA SEKHAN KUTUA JANGWANI

FEI TOTO ATOA NENO HILI BAADA YA SEKHAN KUTUA JANGWANI

Kiungo wa zamani wa Yanga anayekipiga Azam FC kwa sasa, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amekiri kiungo mpya aliyetua kwenye timu hiyo, Shekhan Ibrahim Khamis ni bonge la mchezaji mwenye kipaji na uwezo mkubwa, lakini akamuonya mapema kwa kumtaka ajipange kwelikweli kwa vile ametua katika timu yenye presha kubwa.

“Shekhan ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa na ana kipaji namuona mbali, natarajia atafanya vizuri akipewa nafasi na atapata mafanikio makubwa ndani yake,” alisema Fei Toto na kuongeza;

“Najua amekuja timu kubwa, anatakiwa kupambana na kuonyesha kile alichonacho bila kujali anaenda kupambana na mastaa gani. Ni mchezaji ambaye nimemshuhudia ni mdogo wangu ameanza kujulikana sasa, lakini ni mchezaji ambaye amekuzwa na kufanywa bora chini ya JKU amepita kwenye misingi ya soka hivyo naamini atakuwa bora.”

SOMA NA HII  ISHU YA BEKI WA AZAM FC MORRIS KUJIUNGA NA SIMBA IPO NAMNA HII