Home Habari za michezo MAMBO HADHARANI ISHU YA YANGA KUFANYA KIINGILIO BURE

MAMBO HADHARANI ISHU YA YANGA KUFANYA KIINGILIO BURE

Habari za Yanga SC

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka EA Radio, Ibra Kasuga amefunguka kuhusu Klabu ya Yanga kuamua mashabiki zake waingie bure kwenye mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Medeama FC.

Katika mchezo huo utakaopigwa Jumatano, Desemba 20, 2023 katika Dimba la Mkapa, mfadhili wa Yanga, Ghalib Said Mohammed amenunua tiketi zote za jukwaa la mzunguko, hivyo mashabiki wataingia bure.

“Mechi dhidi ya Medeama sio mechi ya kwanza kwenye hatua ya makundi kwa Yanga, kwa mechi za nyumbani hii ni mechi ya pili, kwa hiyo inategemea mechi iliyopita wameona nini.

“Mechi iliyopita ilikuwa na kiingilio inawezekana waliona hadi dakika ya mwisho kuna kusuasua basi safari hii wamenunua, lakini pia wanaangalia trend ya mashabiki kuingia uwanjani.

“Tangu msimu huu umeanza kwenye Tamasha la Yanga Day wanaangalia je namba ya watu inakuwa kubwa au inakuwa ndogo? kama ni kubwa vizuri ila kama ni ndogo hatutaki picha yenye mapengo. Mwisho wa siku lazima uingie mfukoni,“ amesema Ibra.

SOMA NA HII  GAMONDI AWASOMA WAPINZANI WA SIMBA KWA MBALI