Home Uncategorized KUMBE KOCHA WA YANGA ALITAKA KUJA BONGO MIAKA MINNE ILIYOPITA

KUMBE KOCHA WA YANGA ALITAKA KUJA BONGO MIAKA MINNE ILIYOPITA


KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael,amesema kuwa alikuwa ana mpango wa kuja Bongo miaka minne iliyopita lakini mambo hayakuwa kama alivyotarajia akabaki Afrika Kusini. 

Kwa sasa Eymael anakiongoza kikosi cha Yanga ambacho kinashiriki Ligi Kuu Bara akipokea kijiti cha aliyekuwa Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera ambaye alipigwa chini kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni mwenendo mbovu wa timu.

Eymael amesema :”Nilikuwa nina mpango wa kuja Bongo miaka minne iliyopita kuifundisha Yanga, sababu kubwa nilikuwa napenda kuja Tanzana ila mambo hayakwenda sawa.

“Kwa sasa nipo ndani ya Yanga ninaendelea na maisha na kuna mengi ambayo ninayafanya ila yote kwa yote ninafurahi kuwa Tanzania,” amesema Eymael.

SOMA NA HII  JUMA ABDUL, YONDANI MAMBO SAFI YANGA, DANTE MAMBO BADO