Home Uncategorized PILATO SITA WATANGAZWA KWA KAZI MAALUM KESHO SIMBA NA AZAM NGAO YA...

PILATO SITA WATANGAZWA KWA KAZI MAALUM KESHO SIMBA NA AZAM NGAO YA JAMII


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza marefa sita ambao watachezesha mchezo wa kesho wa Ngao ya Jamii kati ya Simba na Azam FC, mchezo ambao utachezwa kuanzia majira ya saa 1:00 usiku kwenye uwanja wa Taifa.

Mwamuzi wa kati atakuwa Elly Ally Sassi ( Hery Sasii) kutoka Dar atasaidiwa na Frank John Komba, Mwamuzi Msaidizi namba moja (Line 1) wa Dar, Mwamuzi Msaidizi namba mbili (Line 2) atakuwa Mohamed Mkono kutoka Tanga.

Mwamuzi wa akiba (Forth Official) atakuwa Ferdinand Chacha kutoka Mwanza huku Jonesia Jackson Rukiyaa kutoka Kagera atakuwa msaidizi upande wa goli la kwanza na Martin Saanya wa Morogoro atakuwa msaidizi upande wa goli namba mbili.

Hii itakuwa mechi ya pili Tanzania kuchezeshwa na marefa 6 baada ya ile fainali ya Azam Sports Federation Cup.

Imeandaliwa na Yossima Jr

SOMA NA HII  MBEYA CITY V SIMBA NGOMA NZITO LEO SOKOINE