Home Uncategorized HAPA NDIPO TATIZO LA YANGA LILIPOJIFICHA

HAPA NDIPO TATIZO LA YANGA LILIPOJIFICHA


 KOCHA Mkuu wa Yanga Mserbia, Zlatko Krmpotic amesema kuwa tatizo kubwa la timu yake kwa sasa lipo kwenye safu ya ushambuliaji.

 

Mserbia huyo alikisimamia kikosi hicho kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Prisons uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 akiwa amekaa kwa mara ya kwanza kwenye benchi kuifundisha timu hiyo, tangu akabidhiwe majukumu hayo akimrithi Mbelgiji, Luc Eymael.


Safu ya ushambuliaji ya Yanga hivi sasa inaundwa na Michael Sarpong, Yacouba Songne, Carlos Fernandez ‘Carlinohs’, Tuisila Kisinda na Ditram Nchimbi.

 

 Krmpotic amesema kuwa ameamua kufanya hivyo kutokana na kuona kwamba eneo hilo linatengeneza nafasi za kufunga lakini wanashindwa kuzifanyia kazi kama ilivyokuwa kwenye mechi yao na Tanzania Prisons.

 

“Tunahitaji kufanya marekebisho katika eneo letu la ushambuliaji kwani nimeona kuna upungufu. Tunatengeneza nafasi lakini bado tunashindwa kuzifanya kuwa mabao.Hivyo nimeona tulifanyie kazi eneo hilo kwa kuhakikisha kwamba linazalisha mabao mengi tofauti na ilivyokuwa katika mechi yetu ile ya kwanza na naamini tutafanikiwa,” amesema Krmpotic.

 

Kwa sasa Yanga inajiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Mbeya City inayonolewa na Kocha Mkuu, Amri Said utakaochezwa Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA IHEFU FC KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA SIMBA