Home Uncategorized TAIRONE YULE BEKI MBRAZILI WA SIMBA AMETOA YA MOYONI

TAIRONE YULE BEKI MBRAZILI WA SIMBA AMETOA YA MOYONI


BEKI wa Simba, Mbrazili, Tairone Santos da Silva, amefichua kilichopo moyoni mwake kipindi hiki ambacho Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano mingine hapa nchini kusimama.

Mbrazili huyo mwenye bao moja katika Ligi Kuu Tanzania Bara, amesema anatamani kuona anashinda ubingwa akiwa na jezi za timu hiyo.

Mbali na kutwaa ubingwa, Tairone amewakumbuka mashabiki wa soka hasa wale wa Simba ambao walikuwa wakiwapa sapoti katika mechi zote 28 za Ligi Kuu Tanzania Bara ambazo wamecheza mpaka sasa na kuwa kileleni na pointi zao 71 kibindoni.

“Nimewakumbuka mashabiki wetu na kushangilia ushindi pamoja na wachezaji wenzangu. Nataka kushinda ubingwa nikiwa na Simba,” alisema Tairone.

SOMA NA HII  KOCHA BORA MWEZI OKTOBA, KAZE AWAPA TANO WACHEZAJI WAKE