Home Uncategorized JUMA KASEJA:WACHEZAJI WENGI VIWANGO VITAPOROMOKA

JUMA KASEJA:WACHEZAJI WENGI VIWANGO VITAPOROMOKA

JUMA Kaseja kipa mkongwe ndani ya ardhi ya Bongo anayekipiga ndani ya Klabu ya KMC amesema kuwa wachezaji wengi wameshuka viwango kutokana na kukaa muda mrefu bila kucheza. 

Machi 17,2020 Serikali ilizuia mikusanyiko isiyo ya lazima pamoja na ligi zote kusimamishwa kutokana na mlipuko wa Virusi vya Corona ambavyo vinaivurugavuruga dunia.

Kaseja amesema:”Mchezaji yeyote atakayekaa nje ya Uwanja zaidi ya mwezi mmoja bila kucheza na kufanya mazoezi ya nguvu lazima kiwango chake  kitaporomoka hivyo wachezaji wengi wamekumbwa na hali hiyo kwa kuwa wamekaza muda mrefu bila kucheza.

 “Wachezaji wengi wamekosa mazoezi na mechi nyingi naona kutakuwa na ngumu sana kama Ligi ikirejea tena kwani kutakuwa na kazi ya ziada kwa wachezaji kurejesha viwango vyao.”

SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR YAACHANA NA ISHU YA GHARAMA WALIZOTUMIA TANGA