Home Uncategorized NYOTA SABA WA YANGA WAIBUKIA UTURUKI

NYOTA SABA WA YANGA WAIBUKIA UTURUKI

BAADA ya kumaliza Dar Dabi, Uwanja wa Mkapa Novemba 7 kwa sasa maisha ya wachezaji wa Yanga yapo Uturuki ambapo wameweka kambi ya siku tatu.


Stars chini ya Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije ipo kwenye maandalizi ya mchezo wa kuwania kufuzu Afcon dhidi ya Tunisia.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Novemba, 13, nchini Tunisia na nyota saba wa Yanga wamejumuishwa ndani ya kikosi hicho.


Uwanja wa Mkapa ngoma ilikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 na hawa hapa nyita wa Yanga wapo ndani ya kikosi cha Stars:-Metacha Mnata, Deus Kaseke, Bakari Mwamnyeto, Abdallah Shaibu (Ninja), Ditram Nchimbi, Feisal Salum na Farid Mussa wote wa Yanga.


SOMA NA HII  KOCHA COASTAL UNION ASHUSHA PRESHA MASHABIKI