Home Habari za michezo “KUNA WATU WAMEWEKEZA PESA WANA…MICHAMBO,MASIMANGO NA MINUNO”…ALLY KAMWE

“KUNA WATU WAMEWEKEZA PESA WANA…MICHAMBO,MASIMANGO NA MINUNO”…ALLY KAMWE

ALI KAMWE LOLOTE LITAFANYIKA MWARABU AFE...TUNGULI RUKSA...DUA RUKSA

Zikiwa zemesalia siku chache ambapo Klabu ya Yanga itakutana na Rivers United kutokea nchini Nigeria katika mechi ya marudiano Kombe la Shirikisho CAF,

Afisa habari wa klabu hio amwaga tambo zake kuwahakikishia wadau na mashabiki wa timu hio uhakika wa kutinga hatua ya Nusu Fainali.

Mechi hiyo Yanga atakuwa mwenyeji wa mchezo akimualika Rivers United kwenye Dimba la Mkapa, Jumapili, Aprili 30, 2023.

“Ghalib ni Bilionea ambaye amewekeza kwa muda mfupi na timu inakaribia kwenda nusu fainali, kuna watu wamewekeza pesa, masimango, vichambo, minuno na kila aina ya gubu na wanaishia robo fainali,” amesema Ally Kamwe.

SOMA NA HII  YANGA NAO WAONJA LADHA YA USHINDI