Home Habari za michezo IMEFICHUKA!!!….MAYELE KUTWAA KIATU CHA DHAHABU…KOMBE LA SHIRIKISHO

IMEFICHUKA!!!….MAYELE KUTWAA KIATU CHA DHAHABU…KOMBE LA SHIRIKISHO

Tetesi za Usajili Yanga

Afisa Habarai wa Klabu ya Yanga, Alikamwe amesema kuwa
Mshambuliaji wa timu hiyo Fiston Mayele amewaambia wachezaji wenzake wamsaidie kupata kiatu cha dhahabu cha ufungaji bora wa Kombe la Shirikisho.

“Fiston Mayele ana goli tano (5) Kombe la Shirikisho Afrika, akiwa kwenye chumba cha kubadilishia nguo amewaambia wachezaji wenzake, kwa mara ya kwanza na ninyi mkanisaidie kiatu cha Ufungaji Bora.

Kamwe ameongeza “Fiston amewataka wenzake sasa wamsaidie ndiyo maana ‘assists’ zinaanzia nyuma, usishangae na kipa Diarra na yeye akapanda kwenda kumtengenezea Mayele,” amesema Ally Kamwe

Yanga itakutana na Rivers United kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika mchezo wa pili siku ya Jumapili katika Uwanja wa Benjamin Mkapa wakiwa na faida ya goli 2-0 walizopata Nigeria.

SOMA NA HII  USAJILI WA SIMBA WASHTUA...KOCHA MPYA ASHIKILIA MAFAILI YA MASTAA HAWA