Home Uncategorized NYOTA WAWILI YANGA KUIBUKIA TP MAZEMBE YA CONGO

NYOTA WAWILI YANGA KUIBUKIA TP MAZEMBE YA CONGO

 


KIUNGO mzawa ndani ya kikosi cha Yanga,  Feisal Salum wengi wanapenda kumuita Fei Toto ameingia Kwenye anga za Klabu ya TP Mazembe ya Congo.


Mbali na Toto pia beki mzawa wa kati  Bakari Mwamnyeto anatajwa kuingia kwenye rada za vigogo hao wa soka ndani ya Afrika. 


Wazawa hawa wote wawili wana nafasi ya kucheza timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na kwenye mchezo uliopita wa kufuzu Afcon dhidi ya Tunisia Uwanja wa Mkapa walikuwa na kikosi.


Fei Toto alifunga bao lililoipa pointi moja Stars kwenye sare ya kufungana bao 1-1 huku Mwamnyeto akipambana na Watunisia hao kwa dakika 90.

Ikiwa dili lao litajibu ndani ya Yanga kuna uwezekano wa nyota hawa wawili kusepa ndani ya Yanga ili wakapate changamoto mpya nje ya Bongo.

Ofisa Habari wa Yanga,  Hassan Bumbuli amesema kuwa kwa sasa bado wanajadili juu ya ofa ambazo zimewafikia mezani ili waweze kutoa taarifa kwa mashabiki.

SOMA NA HII  Wachezaji waliokamilisha usajili Ligi Kuu 2019/20