Home Uncategorized MAZEMBE YAWAFUATA FEI TOTO, TSHABALALA DAR

MAZEMBE YAWAFUATA FEI TOTO, TSHABALALA DAR


KIGOGO wa TP Mazembe yupo Jijini Dar es Salaam kufanya mazungumzo ya awali na Simba na Yanga. Si hao tu pia wanazungumza na wakala wa straika wa Serengeti Boys, Kelvin John ‘Mbappe’.

Habari za uhakika ambazo Spoti Xtra imezipata kutoka kwa mmoja wa viongozi wa Yanga ni kwamba, Mazembe wanawataka wachezaji hao watatu kwa mpigo lakini mazungumzo yako kwenye hatua za awali.

Habari zinasema kwamba tayari wameshazungumza na Yanga na Simba kwa nyakati tofauti na leo huenda wakafikia muafaka na wiki ijayo wakamaliza dili.

“Wanataka wachezaji wote watatu na wiki ijayo huenda ukasikia habari njema kwani huo usajili unaeza kumalizika na watakuwa wamefikia muafaka,” alidokeza kiongozi mmoja wa Yanga licha kutotaka kutajwa jina lake kwa madai kwamba ishu hiyo ipo kwenye hatua za awali sana.

Fei Toto amekuwa mhimili wa Yanga katika Ligi Kuu msimu uliopita na sasa yupo Taifa Stars kwenye Afcon.

Tshabalala alifanya vizuri na Simba kwenye michuano ya kimataifa msimu uliopita pamoja na ligi ya ndani huku Mbappe akiwa ndiye straika namba moja wa Serengeti Boys na mchezaji anayetajwa kufuata nyayo za Mbwana Samatta.

SOMA NA HII  KUHUSU SHIBOUB KURUDI SIMBA..UKWELI WA MAMBO HUU HAPA..!!