Home Uncategorized Tusimlaume FEI TOTO, Tatizo liko hapa !

Tusimlaume FEI TOTO, Tatizo liko hapa !

Jana tulikuwa na mechi ya kwanza ya mashindano ya Afcon baada ya kukaa miaka 39 bila kushiriki michuano hii mikubwa barani Afrika.

Kwa bahati mbaya mechi yetu ya kwanza ilikuwa dhidi ya Senegal, timu ambayo ni kubwa sana kwetu na timu ambayo ni bora katika bara la Afrika.

Matokeo yaliyotokea yalikuwa ni matokeo ambayo yalitegemewa kwa sababu Senegal imeizidi sana Tanzania katika maendeleo ya mpira wa miguu.

Pamoja na kufungwa jana, wachezaji wetu ambao tulikuwa tunawategemea kufanya vizuri kutokana na viwango vyao kwenye ligi, lakini walifanya vibaya.

Faisal Salum “Fei Toto” ni mmoja ya watu ambao walicheza katika kiwango cha chini jana. Alikuwa anapoteza mipira kila alipokuwa anapata, hakuwa na uwezo wa kukaa na mpira kwenye miguu yake kwa muda mrefu.

Hili siyo kosa lake kabisa, hili kosa limeanzia kwetu sisi, kwenye ligi yetu. Ligi yetu imekuwa ligi ambayo ni rahisi sana mchezaji kuwa huru kila akipata mpira kwa sababu tu ni ligi ambayo ina uwazi sana (spaces).

Ni ligi ambayo hakuna hardpressing, mara nyingi mchezaji kila akipata mpira huwa anakuwa huru wala hagasiwi na wachezaji wa timu pinzani.

Hii ni tofauti na kwenye mechi ya jana ambapo tulikutana na wachezaji ambao hawatoi uhuru kwa mchezaji kuwa huru kila anapokamata mpira.

Ndiyo maana Faisal Salum “Fei Toto” alipokuwa anakamata mpira hakuwa huru kama alivyozoea kuwa kwenye ligi yetu, alikuwa anagasiwa sana na kupoteza mipira mingi.

Kwa hiyo tatizo linaanzia kwenye ligi yetu. Ligi yetu haitoi nafasi kwa wachezaji wetu kukua katika mazingira ya kushindana na wachezaji wakubwa.

The post Tusimlaume FEI TOTO, Tatizo liko hapa ! appeared first on Kandanda.

SOMA NA HII  Mechi yetu na Azam FC ilikuwa ya kirafiki- Zahera