Home Simba SC SIMBA YATAJA KILICHOWAFANYA WAKASHINDWA KUPATA MATOKEO MBELE YA YANGA

SIMBA YATAJA KILICHOWAFANYA WAKASHINDWA KUPATA MATOKEO MBELE YA YANGA


 JOHN Bocco, nahodha wa Simba amesema kuwa sababu iliyowafanya wapoteze mchezo wao wa jana ni kushindwa kutumia nafasi ambazo walizitengeneza.

Ikiwa inanolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 0-1 Yanga katika mchezo wa Kariakoo, Dabi uliokuwa na ushindani mkubwa.

Bocco amesema:”Ilikuwa ni mchezo mkubwa na wenye ushindani ila mwisho wa siku tumeshindwa kupata matokeo mchezo umeisha tunatazama mechi zetu zijazo.

“Haikuwa kazi rahisi nasi tulikuwa tunahitaji pointi tatu hata wapinzani wetu wanahitaji pointi tatu ambazo wamezipata hivyo tutajipanga kwa ajili ya mechi zetu zijazo,” amesema.

Bocco ni mzawa namba moja kwa utupiaji akiwa ametupia mabao 14 sawa na Prince Dube wa Azam FC ambaye ni raia wa Zimbabwe.

SOMA NA HII  SIMBA:TULICHEZA VIBAYA MBELE YA YANGA