Home Uncategorized ASTON VILLA YAMPIGA CRYSTAL PALACE 2-0

ASTON VILLA YAMPIGA CRYSTAL PALACE 2-0


MAHMOUD Hassan’Trezeguet’ leo amibuka shujaa kwenye mchezo wa Ligi Kuu England mbele ya Crystal Palace kwa kupachika mabao yote mawili yaliyoipa pointi tatu muhimu Villa.

Nyota huyo alianza kucheka na nyavu dakika ya 45+4 na bao la pili alifunga dakika ya 59 na kuwafanya waibuke na ushindi huo baada ya kutoka kupoteza mchezo wao uliopita mbele Manchester United kwa kufungwa mabao 3-0.

Ushindi huo unaifanya Aston Villa kufikisha jumla ya pointi ya 30 ikiwa nafasi ya 18 huku ikiwa imecheza mechi 35 


Mchezo wake unaofuata itakuwa dhidi ya Everton utakaopigwa Julai 16, Samatta alitumia dakika 80 kwenye mchezo wa leo uliokuwa na ushindani mkubwa na nafasi yake ilichukuliwa na Keinan Davis.

SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR: TUNAICHAPA SIMBA NA POINTI TATU TUNASEPA NAZO