Home Uncategorized SIMBA YAIPIGA YANGA 4G, SASA KUKUTANA NA NAMUNGO

SIMBA YAIPIGA YANGA 4G, SASA KUKUTANA NA NAMUNGO


USHINDI wa mabao 4-1 ambao wamepata Simba leo, Julai 12 mbele ya Yanga kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali wa Kombe la Shirikisho unawapa nafasi ya kukutana na Namungo FC kwenye mchezo wa fainali unaotarajiwa kuchezwa Agosti 2, Sumbawanga. 

Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck imepata ushindi huo kupitia kwa Gerson Fraga dakika 21, Clatous Chama dakika ya 50, Luis Miqussone dakika ya 52 na Mzamiru Yassin dakika 88.


Yanga ilipata bao la kufuta machozi dakika ya 70 kupitia kwa Feisal Salum aliyepiga shuti lililomshinda Aishi Manula mlinda mlango namba moja wa Simba.


Namungo FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Hitimana Thiery ilikuwa ya kwanza kutinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa bao 1-0 mbele ya Sahare All Stars. 


Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga ulikuwa na ushindani mkubwa na bao lilipatikana kipindi cha pili kupitia kwa Edward Manyanya.


Luis Miqussone,  kiungo wa Simba amesema kuwa ushindi walioupata ni zawadi kwa mashabiki pamoja na uongozi kiujumla.

SOMA NA HII  TIMO WERNER AKUBALI KUIBUKA CHELSEA