Home Uncategorized Dili la Ajibu limefufuka, TP Mazembe warudi tena

Dili la Ajibu limefufuka, TP Mazembe warudi tena

Baada ya TP Mazembe kuachana na usajili wa Ibrahim Ajib Migomba wiki hii kwa madai ya kutoelewana wao na mchezaji.

TP Mazembe wamerudi tena upya kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Ibrahim Ajib tena kwa Mara nyingine tena.

Inasemekana mwanzoni TP Mazembe walitoa of a ya mshahara wa Dola za kimarekani 4,000 kwa mwezi, mshahara ambao Ibrahim Ajib aliukataa.

Kwa taarifa za ndani zinadai kuwa TP Mazembe wamerudi tena kwa mara ya pili na ofa mpya ya mshahara tofauti na ofa ya kwanza.

TP Mazembe imekuja na ofa ya mshahara wa dola za kimarekani 5,000 kwa mwezi. Kinachosubiriwa ni Ibrahim Ajib kuwasikiliza tena TP Mazembe.

The post Dili la Ajibu limefufuka, TP Mazembe warudi tena appeared first on Kandanda.

SOMA NA HII  GSM YAANZA NA NYOTA HUYU,NDANI YA CHAMPIONI JUMATATU