Home Uncategorized FRANK LAMPARD MAJANGA HUKO ULAYA

FRANK LAMPARD MAJANGA HUKO ULAYA


NDOTO za Frank Lampard kuipandisha timu yake ya Derby County kwenye Ligi Kuu England ziliyeyuka baada ya timu yake kulizwa na Aston Villa mabao 2-1 kwenye fainali ya mtoano wa Ligi Daraja la Kwanza England iliyochezwa kwenye Uwanja wa Wembley, juzi. 

Lampard, ambaye ni staa wa zamani wa Chelsea, alikuwa anapewa nafasi kubwa ya kuipeleka Derby County na kuzidi kupandisha chati yake kwenye ukocha.

Hata hivyo, mabao ya Aston Villa yaliyopachikwa na Anwar El Ghazi na John McGinn yalizima ndoto za Derby County. 

Kocha wa Aston Villa, Dean Smith sasa amejizolea sifa kutokana na kuipandisha timu hiyo, ambayo inaundwa na yosso wengi. 

Villa sasa inaungana na Sheffield United na Norwich City kupanda daraja kushiriki Premier msimu ujao.

Kitendo hicho cha Lampard kushindwa kuipandisha Derby kinaweza kumpunguzia sifa ya kuwaniwa na Chelsea, ambayo inasemekana ilikuwa inafuatilia maendeleo yake kwa karibu ili kumpa nafasi ya kuinoa timu hiyo.

SOMA NA HII  YANGA YA GAMONDI SASA MBELE YA SIMBA CAFCL