Home Uncategorized KOCHA TANZANIA PRISONS: HAIKUWA MALENGO KUGAWANA POINTI MOJAMOJA NA YANGA

KOCHA TANZANIA PRISONS: HAIKUWA MALENGO KUGAWANA POINTI MOJAMOJA NA YANGA


 SALUM Mayanga, Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons amesema kuwa haikuwa hesabu zake kulazimisha sare mbele ya Yanga ila wachezaji wake walizidiwa mbinu mwishoni jambo lililowafanya wakaruhusu bao.


Prisons ilianza kupata bao la kuongoza dakika ya 52 kipindi cha pili kupitia kwa Jumanne Elifadhili liliwekwa sawa na Saido Ntibanzokiza dakika ya 76.

Sare hiyo inaifanya Tanzania Prisons isepe na pointi mbili jumla kwenye mechi mbili mbele ya Yanga ambapo ule wa kwanza Uwanja wa Mkapa zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

Pia mchezo wa kwanza Prisons ilianza kufunga kupitia kwa Lambart Sabiyanka na mchezo wa jana, Desemba 2020 Prisons ilianza kufunga na bao likasawazishwa.

Mayanga amesema:”Ilikuwa tunazihitaji pointi tatu kwa kuwa ilikuwa ni muhimu kwetu kushinda kwa kuwa tumepata sare basi hatuna chaguo.

“Tutajipanga kufanya vema wakati ujao kwenye mechi zetu zijazo, kikubwa mashabiki waendelee kutupa sapoti na tunawashukuru kwa kuwa pamoja nasi.

“Wachezaji pia wanastahili pongezi kwa kuwa walipambana kusaka matokeo mwisho wa siku wakapata pointi moja,” . 

SOMA NA HII  KILICHO NYUMA YA MAFANIKIO YA SIMBA CHAFICHULIWA NA MSHAMBULIAJI WAO NAMBA MOJA