Home Uncategorized NYOTA YANGA ATUMA MAOMBI YA UVUMILIVU

NYOTA YANGA ATUMA MAOMBI YA UVUMILIVU


BEKI ya Yanga, Juma Abdul amewataka wanachama wa klabu hiyo kutulia na kutokatishwa tamaa na matokeo wanayoyapata uwanjani kwa kuwa ndiyo kwanza timu hiyo inajengwa.

Juzi Yanga ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Azam FC kwenye mechi iliyopigwa Uwanja wa Taifa, matokeo hayo yakija baada ya mchezo uliopita kuchapwa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar.

Akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya timu hiyo kukubali kipigo cha pili mfululizo wakiwa chini ya Mbelgiji Luc Eymael, alisema kwa sasa bado hawajauzoea mfumo wa kocha huyo mpya ambaye hiyo ni mechi yake ya pili tangu atue.

“Ninaomba mashabiki wetu waendelee kutupa ushirikiano, wasikatishwe tamaa na matokeo yaliyopita, kidogo kidogo tutamzoea kocha wetu,” alisema Abdul.

 Akizungumzia mchezo huo dhidi ya Azam FC ambao waliibuka na ushindi baada ya beki Ally Mtoni Sonso kujifunga, alisema walifanya makosa yaliyosababisha kukosa pointi tatu muhimu walifanya makosa yaliyosababisha kukosa pointi tatu muhimu.

Alisema mchezo huo ulikuwa mgumu na wenye ushindani mkubwa, ambapo wapinzani wao walitoa presha kubwa langoni mwao na kubahatika kupata bao hilo.

“Wenzetu walitumia nafasi zao vizuri wakatoka na pointi tatu mpira ndivyo ulivyo, kikubwa tunajipanga kwa ajili ya mchezo ujao,” alisema.

Alisema kwa sasa wanajipanga kukutana na timu ya Singida United kesho kutwa katika mchezo utakaopigwa mkoani Singida. Alisema amejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo akiwa na lengo la kuipa ushindi timu yake.

Matokeo hayo yameifanya Yanga kukaa katika nafasi ya saba ikiwa na alama zake 25 baada ya mechi 14, wakati Azam iliyoshuka dimbani mara 15 na kukusanya alama 32, ikikaa katika nafasi ya pili nyuma ya vinara Simba wenye pointi 41 zilizotokana na mechi 16 msimu huu.
SOMA NA HII  WAAMUZI HAKUNA HAJA YA KUPEPESA MACHO, WACHEZAJI KAZI MOJA KUPAMBANA