Home Habari za michezo AHMED ALLY:- “MTASHANGAA SANA…..KAZI NDIO KWAANZAAA INAANZA….”

AHMED ALLY:- “MTASHANGAA SANA…..KAZI NDIO KWAANZAAA INAANZA….”

Habari za Simba leo

Uongozi wa Simba SC umeweka wazi kuwa watawashtua wengi kwa mashine za maana watakazoshusha kupitia usajili wao wa dirisha dogo, ambao umelenga kuboresha kikosi hicho kwenye mechi za ushindani.

Ipo wazi kwamba 2023 Simba SC ilifunga kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukisoma KMC 2-2 Simba SC, na mabao yalifungwa na Saido Ntibanzokiza na Jean Baleke ambaye kafikisha mabao 8 kwenye ligi, yale ya KMC yalifungwa na Wazir Junior.

Meneja wa Habari na Mawasiliana Simba SC, Ahmed Ally amesema kuwa mpaka Januari 15 watakuwa wameshatambulisha wachezaji wapya ambao watakuwa kwenye kikosi hicho kwa ajili ya kuongeza nguvu.

“Kwenye usajili wetu wa dirisha dogo nina uhakika tutawashtua wengi kutokana na aina ya wachezaji ambao tutawatambulisha, hawa wanakuja kufanya kazi kweli, ukizingatia kwamba dirisha dogo halihitaji kusajili wachezaji wengi.

“Maboresho ambayo yanafanyika kwenye dirisha dogo ni maalumu kuongeza nguvu maeneo ambayo hayakuwa imara kidogo kutokana na sababu mbalimbali lakini tutawambulisha wachezaji wapya kabla ya Januari 15 mashabiki watawatambua,’ amesema

Tayari Simba imetoa zawadi ya mwaka mpya 2024 kwa mashabiki wake baada ya kumtambulisha nyota mpya, Salehe Karabaka ambaye anakuwa ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa ndani ya klabu hiyo ya Msimbazi kupitia dirisha hili dogo.

SOMA NA HII  KUELEKEA MICHUANO YA CAF...YANGA WAANZA KUJITUTUMUA MAPEMA...INJINIA HERSI AIBUKA NA TAMKO HILI LA KIBABE...