Home Habari za michezo KUHUSU MZIGO AMBAO SIMBA NA YANGA ZITAPA CAF…UKWELI HUU HAPA…PESA ZAONGEZWA…

KUHUSU MZIGO AMBAO SIMBA NA YANGA ZITAPA CAF…UKWELI HUU HAPA…PESA ZAONGEZWA…

Habari za Simba na Yanga

Simba imeng’olewa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, lakini taarifa njema kwano ni kule kuongezwa mkwanja ikijihakikisha kuvuna Dola 900,000 (zaidi ya Sh 2 Bilioni) baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuongeza mzigo wa fedha za zawadi kwa michuano ya msimu huu.

Ongezeko hilo la fedha halijainufaisha Simba tu, bali hadi watani wao, Yanga ambao imetinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwani hadi sasa ina uhakika wa kuvuta Dola 1 Milioni (zaidi ya Sh 2.35 Bilioni, badala ya 1.8 Bilioni zilizokuwa kwenye kiwango cha zawadi cha awali ikimaliza ya pili.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi jioni kwenye mtandao wa CAF, ni kwamba zawadi za msimu huu zimeboreshwa kwa asilimia 40 ikiwa ni utekelezaji wa ratifa zilizowahi kutolewa na Rais wa Shirikisho hilo, Dk Patrice Motsepe mapema mwaka huu juu ya ongezeko hilo.

Kwa mujibu wa viwango vya sasa vya zawadi hizo kwa Ligi ya Mabingwa, Bingwa anazoa Dola 4 Milioni (zaidi ya Sh 9.4 Bilioni), huku anayemaliza wa pili atanyakua Dola 2 Milioni (zaidi ya Sh 4.7 Bilioni) na zile zilizoingia nusu fainali zinakomba Dola 1.2 Milioni ( zaidi ya Sh 2.8 Bilioni) na zile za robo ambayo Simba nayo ipo hapo ni Dola 900,000 ( zaidi ya Sh 2.1 Bilioni).

Mkwanja wa Simba iliyotolewa na watetezi wa taji hilo Wydad Casablanca ambayo imetinga tena Fainal baada ya kuwaondoa  Mamelodi Sundowns katika mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa upande wa Yanga iliyotinga nusu fainali hadi sasa ina uhakika wa kuzoa Dola 1 Milioni ( zaidi ya Sh 2.35 bilioni). Awali timu iliyotinga fainali na kumaliza kama mshindi wa pili ilikuwa ikizoa Dola 800,000 (zaidi ya Sh 1.8 Bilioni).

Bingwa wa Shirikisho msimu huu inasalia kama ilivyokuwa awali ya Dola 2 Milioni ( zaidi ya Sh 4.7 Bilioni), huku zile zilizotuinga nusu fainali zinakomba kila moja Dola 750,000 (zaidi ya Sh 1.7 Bilioni) na zile zilizokwamia robo fainali zinazoa Dola 550,000 (zaidi ya Sh 1.29 Bilioni).

Yanga ilitinga fainali ikiitoa Marumo Gallants ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 4-1 baada ya kushinda 2-0 nyumbani na kuifunga tena ugenini 2-0 na itavaana hatua hiyo ya sasa na USM Alger ya Algeria mechi ya kwanza ikitarajiwa kupigwa Mei 28 jijini Dar es Salaam na marudiano Juni 3 jijini Algers ili kupata bingwa wa taji hilo lililokuwa mkononi mwa RS Berkane ya Morocco.

SOMA NA HII  HIVI HAPA VIGINGI VITANO VYA SIMBA KWENYE CHAMPIONS LEAGUE 2021